𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐋𝐎𝐑𝐈,𝐋𝐀𝐔𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐔 𝟏𝟏 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐀.
Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo Kijiji cha Chang'ombe Kata ya Segera wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi aina ya Tata kupinduka na baadaye wananchi kujitokeza kusaidia ndipo lori linalodaiwa kufeli breki likawagonga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 13, 2025 na kusema miili imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Korogwe.
Comments
Post a Comment