𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐘𝐀 𝐁𝐀𝐒𝐈 𝐋𝐀 𝐅𝐑𝐄𝐒𝐓𝐄𝐑 𝐈𝐍𝐕𝐄𝐒𝐓𝐌𝐄𝐍𝐓 𝐓 𝟑𝟔𝟖 𝐃𝐍𝐃
TAARIFA YA AJALI YA BASI LA FRESTER INVESTMENT T 368 DND
Jana majira ya saa 6 usiku, basi la Frester Investment lenye namba za usajili T 368 DND lililokuwa likifanya safari zake kutoka Bukoba kuelekea Dar es Salaam limepata ajali nje kidogo mwa Jiji la Dodoma, katika eneo la Mtumba. Chanzo cha ajali kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda na taarifa za awali zilizotolewa, hakuna vifo vilivyoripotiwa hadi sasa, lakini baadhi ya abiria wamepata majeraha madogo pamoja na mshituko. Timu za uokoaji zilifika eneo la tukio kwa haraka na kuwasaidia abiria waliokuwa kwenye basi hilo.
Aidha, mamlaka husika zimeanza uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo ili kubaini kwa kina chanzo na kuchukua hatua stahiki. Abiria waliopata majeraha walikimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi, huku wengine wakipewa huduma za kwanza katika eneo la tukio.
Tunatoa pole kwa abiria wote waliopata majeraha na tunaendelea kuwasihi madereva wote kuwa makini barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika. Mamlaka zinaendelea kufuatilia hali ya abiria na kutoa taarifa zaidi kadri uchunguzi unavyoendelea.
Comments
Post a Comment